Hii ni kutoka Manchester United, kutana na mchezaji mwenye kasi kuliko wote…
Beki wa Manchester United, Chris Smalling ni moja kati ya wachezaji ambao wamekuwa wakilaumiwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na ubovu wa safu ya ulinzi ya United ambayo imekuwa ikiruhusu sana mabao kufungwa.
Ni vigumu kuamini kuwa beki huyu ambaye alijiunga na United miaka minne iliyopita leo hii ndio mchezaji mwenye kasi kuliko wote kwa mujibu wa takwimu za klabu hiyo.
Hii ni siri iliyofichuliwa na mshambuliaji wa Manchester United, James Wilson ambaye salisema kuwa kuna wachezaji wengi wenye kasi kwenye timu hiyo lakini hakuna anayemzidi Chris Smalling.
Wilson
amezungumza haya kwenye mahojiano maalum ambapo alisema kuwa wanapokuwa
uwanjani huwa wanavalishwa vifaa maalum vya GPS ambavyo kwa msaada wa
teknolojia ya kisasa humsaidia kocha na wasaidizi wake kutambua jinsi
wachezaji wanavyofanya mazoezi pamoja na kasi waliyo nayo na umbali
ambao wanakimbia.
Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na kifaa hicho hakuna mwenye kasi kama Chris Smalling ndani ya kikosi cha Man United.
James Wilson pia amewataja wachezaji wengine kama Ashley Young, Luke Shaw, Antonio Valencia pamoja na yeye mwenyewe kama wachezaji wengine wenye kasi lakini bado hakuna anayemzidi Smalling.
No comments:
Post a Comment